Zawadi ya jezi kwa 'Legendary'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2022
Zawadi ya jezi kwa 'Legendary'

Katika moja ya mahojiano aliyofanya, winga wa Yanga Denis Nkane aliweka bayana kuwa Mrisho Ngasa ndiye mchezaji aliyekuwa akimvutia zaidi na hakukosa kufika uwanjani kumshuhudia wakati ule akiitumikia Yanga

Nkane ana mambo mengi sana ambayo anafanana na Ngasa, katika umri mdogo Nkane amesajiliwa na Yanga na anapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza

Alipotua Yanga kwenye dirisha dogo mwezi January, Nkane alichagua kutumia jezi namba 16, jezi ambayo amevaa Ngasa katika kipindi chote alichoitumikia Yanga

Leo Nkane amepata nafasi ya kukutana na Ngasa na kumzawadia jezi ya klabu ya Yanga

Ngasa amesema amepewa heshima kubwa na Nkane, akimtakia kila la kheri ili aweze kupata mafanikio pengine hata zaidi ya aliyopata yeye

"Ni Heshima kubwa sana kuvunja majukumu yenu na kuja kunipa zawadi nimeona kweli pia kuna mfanano wa sura zetu nakutakia mambo mazuri na yaliojifunga yafunguke inshallah kwa uwezo wa Allah," aliandika Ngasa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’