Tufikirie mechi mbili za ligi kuu kwanza - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2022
Tufikirie mechi mbili za ligi kuu kwanza - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amewataka wachezaji wa timu hiyo kuweka mawazo yao kwenye mechi za Ligi Kuu zinazowakabili badala ya kufikiria mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba.

Nusu fainali ya Kombe la FA, itazikutanisha timu hizo Mei 28 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kila timu imepania kutaka kushinda mchezo huo ili kucheza fainali.

Kaze amesema mataji yote mawili yapo katika malengo yao lakini kwa sasa wanapaswa kuweka nguvu zao kwenye mechi mbili za ligi zinazowakabili ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutangaza ubingwa kuliko mchezo wa Simba.

"Mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba tunaupa uzito mkubwa lakini kwa sasa wachezaji hawapaswi kuufikiria sababu tuna mechi mbili za Ligi Kuu kabla ya mchezo huo na tunapaswa kushinda ili kujiweka karibu na malengo yetu na baada ya hapo ndio tutaanza kufikiria namna ya kuikabili Simba," alisema Kaze

Kaze amesema licha ya kuwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 10 lakini hicho hakipaswi kuwa kigezo cha kujiamini na kushindwa kuzipa umuhimu mechi zilizobaki kwani pointi walizokuwa nazo bado hazijatosha kuwapa ubingwa

Kesho Ijumaa Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya Kwanza kisha kuelekea mkoani Mwanza kuikabili Biashara United May 23

Kama Yanga itashinda mechi hizi mbili na Simba kukosa ushindi (kufungwa) katika mchezo wao unaofuata dhidi ya Geita Gold, Yanga itatwaa ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’