Baada ya walinzi Kibwana Shomari na Bakari Nondo Mwamnyeto kusaini mikataba mipya ya kuendelea kuwatumikia Wananchi, kiungo Zawadi Mauya nae amesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia Yanga
Moja ya viungo bora katika ligi kuu ya NBC ingawa jina lake halizungumzwi sana
Mauya amekuwa na wakati mzuri tangu aliposajiliwa na Yanga akitokea Kagera Sugar misimu miwili iliyopita
Chini ya kocha Nabi, Mauya ameendelea kuimarika zaidi, akiisaidia Yanga kila anapopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza
Ataendelea kuitumikia Yanga kwa misimu mingine miwili
ADVERTISE HERE