Mlinzi wa kulia wa Yanga Djuma Shabani amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo kwa ajili ya michuano ya kuwania tiketi ya fainali za Afcon 2023 inayoanza mwezi Juni
Djuma ni mchezaji pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki na Kati katika wachezaji kutoka DR Congo walioitwa timu ya Taifa
Sio jambo jepesi kuitwa timu ya Taifa ya DR Congo ambayo ina idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza barani Ulaya
Wakati Djuma akiitwa Congo, mlinda lango Djigui Diarra amejumuishwa timu ya Taifa ya Mali, Khalid Aucho (Uganda) na Saido Ntibazonkiza (Burundi)
Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Farid Mussa, Dickson Job, Bakari Nondo Mwamnyeto, Salum Abubakar na Feisal Salum wao wamejumishwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Wachezaji 11 wa Yanga watakuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa mwezi Juni