Washambuliaji wa zamani wa Yanga Tuisila Kisinda na Fiston Abudulrazak jana wakiwa na RS Berkane, walitwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika
Berkane inayonolewa na kocha wa zamani wa AS Vita, Florent Ibenge, wametwaa taji hilo kwa ushindi wa mikwaju ya penati 5-4 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Orlando Pirates
Kama ulifuatilia michuano hiyo msimu huu, utakubali kuwa hakuna muujiza, inawezekana kabisa kombe hilo na hata lile la ligi ya mabingwa kutua Tanzania
Kama isingekuwa ile changamoto ambayo Yanga walikutana nayo mwanzoni mwa msimu katika michuano ya ligi ya mabingwa wakiondoshwa na Rivers United, kwa kikosi hiki cha kocha Nasreddine Nabi, pengine tungekuwa tukizungumza mengine
Msimu ujao Yanga itaingia katika michuano ya ligi ya mabingwa ikiwa na dhamira ya dhati ya kufanya vizuri


