Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki wa timu hiyo 'kujongea' kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba jioni ya leo kuishangilia timu yao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United
Bumbuli amesema ushindi katika mchezo huo utawapa uhakika wa kutimiza malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu kwani kimahesabu watahitaji alama nyingine moja tu kuwa mabingwa
Mtanange huo utaunguruma kuanzia saa kumi kamili jioni, hesabu ikiwa ni ushindi ili kufikisha alama 66 ambazo Simba itahitaji kushinda mechi zote zilizobaki kuweza kuzifikia
ADVERTISE HERE