Haturudii makosa Iringa - Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2018
Haturudii makosa Iringa - Lwandamina
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, tayari wako mkoani Iringa na benchi la ufundi limesema hawatarudia makosa katika mchezo wao dhidi ya wenyeji Lipuli FC kesho.

Lipuli FC inatarajia kuwakaribisha Yanga katika mechi ya raundi ya 16 itakayofanyika kwenye Uwanja wa Samora uliopo Iringa Mjini.

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amesema kwenye ligi hakuna mechi rahisi na hasa katika hatua ya duru la pili ambalo linatarajia kuanza leo kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Lwandamina alisema kuwa wamejipanga kuona makosa yaliyotokea katika mchezo wa kwanza hayajirudii na kesho wanaondoka na pointi zote tatu.

"Kimahesabu hakuna ambaye anaweza kusema ana nafasi ya kuwa bingwa, ila ili uwe kwenye nafasi ni lazima ushinde mechi zako zote bila kuangalia matokeo ya mpinzani wao, tunaamini tutafanikiwa," alisema kwa kifupi Mzambia huyo.

Naye Kocha wa Lipuli FC, Suleiman Matola, alisema kuwa amewaandaa wachezaji wake kupambana na kutohofia majina ya wachezaji wa Yanga.

"Kitu kikubwa kwenye mpira ni kuwa na utulivu, ukikosa utulivu unamruhusu mpinzani acheze na atawale mchezo, ukitulia na kila mmoja akitekeleza jukumu lake ninaamini tutazibakisha pointi tatu nyumbani, tulipata pointi moja ugenini, sasa ni zamu yetu kutimiliza malengo ya kucheza nyumbani," alisema kiungo na nahodha wa zamani wa Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
34m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
59m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’