Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele jana alifunga goli lake la 14 msimu huu na kumfikia George Mpole wa Geita Gold hivyo 'kunogesha' vita ya washambuliaji hao katika kuwania kiatu cha dhahabu
Mayele amefikia rekodi aliyoweka kwenye ligi kuu ya DR Congo msimu uliopita wakati akiwa na AS Vita
Alimaliza msimu akifunga mabao 14, akishika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora
Mabao yake 14 yaliisaidia AS Vita kutwaa ubingwa DR Congo
Mayale anahitaji kufunga mabao mawili katika michezo minne iliyobaki kufikia rekodi ya mabao 16 ya msimu uliopita
Kwa kuwa Yanga ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa mapema, ni wazi Mayele atakuwa na wakati mzuri wa kusaka kiatu cha dhahabu katika mechi zitakazokuwa ziebaki
ADVERTISE HERE