Sureboy 'anawataka' kwelikweli Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 May 2022
Sureboy 'anawataka' kwelikweli Simba

Kiungo fundi wa Yanga, Salum Aboubakar ameonyesha kuutamani kwelikweli mchezo nusu fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Simba ili wananchi wafurahi.

Baada ya kuukosa mchezo uliopita akipewa dakika chache dhidi ya Simba kwenye ligi, Sureboy anautaka mchezo wa Mei 28 apate muda wa kutosha ili awafanyie kazi bora zaidi mashabiki wa timu hiyo.

Sure Boy ambaye ameanza kutengeneza mabao, alisema anaamini kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi hatakosea akimpa nafasi hiyo akiamini kuwa ubora wa timu hiyo kwasasa utaifanya Yanga kushinda mchezo huo.

"Siwezi kulalamika juu ya muda niliopewa kwenye mechi iliyopita, makocha wanajua zaidi kuliko mimi, ila safari hii namuomba kocha aniamini kwa muda zaidi, mashabiki wa Yanga wanatakiwa kufurahi,". Sureboy amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Kwasasa naijua Yanga, sio kwamba mimi ni bora lakini nacheza na watu bora ambao wananipa wepesi, mimi sio mtu wa kuogopa mechi tunaheshimu tunakwenda kukutana na timu kubwa kama sisi lakini Yanga tupo kwenye ubora na mashabiki wetu wana nguvu ya kutushangilia wakati wote"

Aidha Sureboy pia alizungumzia mwanzo wake bora katika kikosi hicho akisema uwepo wa wachezaji wengi waliokomaa kiakili unampa wakati mzuri kufanya majukumu yake.

"Siwezi kuisema vibaya Azam ile ni timu ambayo imenilea naiheshimu sana lakini kitu tofauti hapa Yanga ni kwamba kuna wachezaji wengi waliokomaa kiushindani, unapopiga pasi unampa mtu ambaye anakwenda kuendeleza kitu kwa ubora sasa hapo lazima mambo yawe rahisi"

"Ushirikiano ni mkubwa sana kwa wenzangu kuanzia mazoezini hadi uwanjani tunapocheza mechi, maisha yetu yamekuwa ya furaha tunafurahia kazi yetu, eneo la namna hiyo lazima mchezaji ufanye makubwa uwanjani"

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika kikosi cha Yanga, Sureboy amerejeshwa kwenye timu ya Taifa ambayo mwezi ujao itaanza kampeni ya kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’