Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amekuwa na msimamo mkali kwa wachezaji wake juu ya umuhimu wa kuzingatia maelekezo wanayopewa pamoja na kuwa na nidhamu
Nabi mwenye uraia pacha wa Tunisia na Ubelgiji, amesema nidhamu ndio silaha ya kupelekea mafanikio katika jambo lolote unalofanya
"Tunatakiwa kufanya mambo yetu Kwa kuheshimu muda hii ndio hatua ya kwanza ya nidhamu. Ukiwa na nidhamu ya kuheshimu muda hata uwanjani utakuwa makini"
"Wachezaji wangu wanafahamu, ukifanya makosa unakumbana na adhabu na hili nalisimamia mwenyewe ili mambo yaende Kwa haraka, " alisema Nabi
Jana uongozi wa Yanga ulithibitisha kusimamishwa kwa wachezaji wawili Saido Ntibazonkiza na Dickson Ambundo ambao waliondoka kambini kinyume na maelekezo baada ya mchezo dhidi ya Biashara United
Wachezaji hao wataukosa mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, May 28 katika uwanja wa CCM Kirumba
Hii sio mara ya kwanza kwa Nabi kuchukua hatua kwa wachezaji wanaokwenda kinyume na taratibu za kambi
Siku chache tu baada ya kujiunga na Yanga msimu uliopita, Nabi alimsimamisha aliyekuwa nahodha Lamine Moro baada ya kuchelewa kufika mazoezini