Kesho Jumamosi, pale uwanja wa CCM Kirumba hapatatosha kwani vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga watakuwa dimbani kuwakabili watani zao Simba katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Ni mtanange unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa jijini Mwanza na mikoa ya jirani ambao hawajazishuhudia timu hizi zikichuana kwa miaka kadhaa sasa
Mauzo ya tiketi yalianza tangu juzi ambapo leo misururu ya mashabiki kununua tiketi imeongezeka katika uwanja wa CCM Kirumba
Tiketi za VIP A zimeshamalizika, mpaka kufikia jioni pengine mauzo ya tiketi yatahitimishwa
Hivyo Mwananchi wa Mwanza unapaswa kuhakikisha umekamata tiketi yako leo, ili kuwashuhudia kina Fei Toto wakifanya yao hapo CCM Kirumba kesho

ADVERTISE HERE