Yanga imekamilisha maandalizi yake kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba
Wananchi walichimbia mkoani Shinyanga na wanatarajiwa kuelekea Mwanza mapema kesho tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa tisa na nusu Alasiri
Msimu huu Yanga imepania kutwaa mataji yote. Walianza na Ngao ya Jamii, wanahesabu siku kabla ya kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya NBC na kesho wamedhamiria kuwaadhibu watani zao Simba na kutinga fainali ya kombe la FA
Yanga itaingia katika mchezo wa kesho ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa fainali ya michuano hiyo msimu uliopita mkoani Kigoma
Utakuwa mchezo wa kisasi kwa Yanga, kwa hakika vijana wa kocha Nasreddine Nabi wamedhamiria kulipa kisasi