Baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika, mkongwe Saido Ntibazonkiza anatajwa kuwa mbioni kujiunga na Singida Big Stars (DTB) ambayo itacheza ligi kuu ya NBC msimu ujao
Klabu hiyo iliyohamishia makazi yake mkoani Singida, pia inatajwa kuwawania nyota kadhaa wa Yanga ambao mikataba yao iko ukingoni
'Mwaisa mtu mbadi' Deus Kaseke nae anaweza kuibukia kwa walima alizeti hao ambao wanatajwa kupita mulemule ilimopita klabu ya Singida United ambayo Kaseke aliwahi kuitumika
Nyota waliowahi kuitumikia Yanga, Juma Abdul, Geofrey Mwashiuya na Amissi Tambwe walikuwa sehemu ya kikosi kilichoipandisha timu hiyo daraja msimu huu
ADVERTISE HERE