Ligi nyingi zikiwa zimemalizika duniani, Yanga imeendelea kuwa klabu pekee ambayo haijapoteza mchezo baada ya kucheza michezo 26
Wananchi wamekaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu wakihitaji alama tatu tu kutoka michezo minne iliyobaki kuhesabu taji la 28 la ligi
Lakini pia Yanga inawania rekodi nyingine ya kibabe msimu huu. Wananchi tayari wamecheza zaidi ya miezi 12 pasipo kupoteza mchezo kwenye ligi sawa na michezo 33
Kama Yanga haitapoteza mchezo katika mechi nne zilizobaki, ina maana watakamilisha idadi ya michezo 37 pasipo kupoteza mchezo
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema dhamira yao ni kuhakikisha wanamaliza msimu huu pasipo kupoteza mchezo
ADVERTISE HERE