Yanga kuweka kambi ya 'kishua'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jun 2022
Yanga kuweka kambi ya 'kishua'

Kama ratiba itakwenda kama inavyopigwa baada ya Yanga kubeba ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la ASFC, kikosi hicho kitasafiri hadi Boston, Marekani kuweka kambi ya msimu mpya wa michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Taarifa ziwafikie mashabiki wa Yanga ambao kwa sasa wananenepa kwa furaha kutokana na chama lao kufanya vyema msimu huu, kuwa bilionea na mfadhili wa Yanga, Ghalib Mohamed 'GSM' amefurahia mafanikio iliyoyapata na anapiga hesabu kambi ya timu hiyo kwa msimu ujao iwe Boston, Marekani kama chaguo lake la kwanza.

Kambi hiyo itakuwa ni maalumu kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu, ASFC na Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo mabosi wanapiga hesabu kufika mbali

Mbali na chaguo hilo, bilionea huyo pia ana machaguo mengine mawili ikiwamo Uturuki na Afrika, huku Sauzi ikilengwa zaidi

"Unajua Ghalib (Said) anaipenda sana Yanga na hatua ya kufikia kuwa na nafasi ya kuchukua mataji mawili tena yote yalitokea Simba imemfurahisha zaidi na anataka timu ikaweke kambi huko Boston," alisema bosi mmoja wa ndani Yanga.

Itakumbukwa msimu uliopita GSM aliipeleka Yanga nchini Morocco katika jiji la kitalii la Marrakech. Hesabu za GSM katika kambi hiyo kwa sasa zinajikita katika ombi la benchi la ufundi ambalo limetaka uhakika wa kupatikana timu nzuri zitakazowapa mazoezi katika mechi za kirafiki kwenye maandalizi hayo.

Benchi la Yanga chini ya kocha Nasreddine Nabi limetaka uhakika huo kutokana na muda mfupi wa kambi.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’