Mambo magumu kwa Tanzania leo ikishindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani na kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Algeria katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023
Mabao ya Rami Bensebain na Mohamed Amoura yalitosha kuihakikishia Algeria ushindi huo ambao unawafanya wajichimbie kileleni mwa kundi F baada ya kufikisha alama sita
Algeria wamenufaika na uzoefu wao, ubora wa kikosi na mchezaji mmoja mmoja. Vijana wa Poulsen walipambana lakini makosa mawili waliyofanya yalitumiwa vyema na Algeria
Bado kuna michezo minne, miwili dhidi ya Uganda na Niger katika uwanja wa Benjamin Mkapa, mmoja dhidi ya Uganda ugenini na mwingine dhidi ya Algeria ugenini
Ni wazi Tanzania, Uganda na Niger zitaingia katika vita kubwa ya kuwania nafasi ya pili, Algeria wana kila dalili watamaliza vinara wa kundi F
Katika mchezo wa mapema kati ya Uganda dhidi ya Niger, matokeo ya mchezo huo yalikuwa sare ya bao 1-1
Niger wako nafasi ya pili kundi F wakiwa na alama mbili wakati Uganda na Tanzania zote zina alama moja huku kila timu ikiwa imeruhusu mabao mawili