Jana Tanzania ilihitimisha mchezo wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023 kwa kupoteza dhidi ya Algeria wakifungwa mabao 2-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya mechi hizo za kalenda ya CAF, sasa tunarejea kwenye ngwe ya lala salama ligi kuu ya NBC pamoja na michuano ya kombe la FA
Kwa Yanga ni awamu ya kumaliza kazi iliobaki kabla ya kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu msimu huu
Yanga inahitaji alama tatu tu, na kama watazipata katika mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union, basi shamra shamra za ubingwa zitaanza
Yanga na Coastal Union zitachuana Jumatano ijayo, Juni 15 katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE