Ni misimu minne kuanzia 2017-18 mpaka 2020-21 Wananchi hawajatwaa ubingwa wa ligi kuu
Lakini ubingwa wanaokwenda kutwaa msimu huu utamaliza machungu ya kuukosa katika misimu hiyo minne!
Ni hivi; thamani ya ubingwa wa Yanga msimu huu ni zaidi ya thamini ya ubingwa katika misimu sita iliyopita kwa pamoja
Msimu huu Wananchi watapata kombe jipya lenye thamani kubwa zaidi pengine kuliko mataji 27 waliyoshinda kabla
Wataondoka na kitita cha Tsh Milioni 600 fedha ambazo ni zaidi ya fedha ambazo watani zao Simba walipata kwa pamoja katika misimu minne mfululizo waliyoshinda ubingwa
Hesabu ziko hivi; msimu wa 2017-18 bingwa alipata Mil 80, 2018-19(Mil 80), 2019-20(Mil 100) na 2020-21 (Mil 100), jumla ya fedha zote walizopata ni Tsh Mil 360
Yaani thamani ya ubingwa wa Yanga msimu huu ni Mil 240 zaidi ya fedha ambazo watani zao walipata katika misimu yote minne kwa pamoja!