Lazarus Kambole mshambuliaji mwenye umri wa miaka 28, alizaliwa nchini Zambia January 20, 1994. Alitengeneza jina lake wakati anaitumikia klabu ya Zesco United kati ya mwaka 2014 na 2019 kabla ya kusajiliwa na Kaizer Chiefs ambayo ameachana nayo hivi karibuni baada ya mkataba wake kumalizika.
Anahusishwa kujiunga na Yanga ambapo imeelezwa wiki hii anaweza kutua nchini kukamilisha usajili wake
Ni mshambuliaji wa kati ambaye pia ana uwezo wa kucheza nafasi ya ushambuliaji akitokea pembeni
Alijiunga na klabu ya Zesco Utd ya Zambia mwaka 2014 na kudumu mpaka 2019, Kambole akiwa Zesco United alicheza micheza 56 na kufanikiwa kufunga mabao 39
Mpaka sasa Kambole anashikilia rekodi ya kufunga hat-trick ya haraka zaidi kwenye historia ya michuano ya klabu bingwa Afrika na hii ilikuwa mwaka 2018 akiwa na klab ya Zesco Utd
Katika msimu huo ambao alikuwa kinara wa mabao ligi ya mabingwa, alifunga mabao (10), mabao (3) kati ya hayo ni hat-trick aliyoifunga klabu ya Mbabane Swallows ndani ya dakika tano
Baada ya misimu hiyo ya mafanikio makubwa akiwa Zesco, klabu ya Kaizer Chiefs ikamsajili katika msimu ambao pia alihusishwa na klabu za hapa nyumbani Yanga na Simba
Kambole akakutana na changamoto katika misimu yote mitatu akiwa Kaizer Chiefs kutokana na ushindani wa nafasi ya kucheza dhidi ya washambuliaji wenzake watano wakiongozwa na SAMIR NURKOVIC kutoka Serbia na Leonardo Castro
Hakuwahi kucheza hata nusu ya mechi (dakika 90) kwa msimu, muda mwingi alikuwa anaanzia benchi (sub)
Haishangazi kuona Mzambia huyo alifunga mabao mawili katika michezo 46, ambapo katika mechi nyingi alizocheza alitumika kama winga
Lakini kwa sababu hakufanya vizuri Afrika Kusini haimaanishi kuwa pia hatafanya vizuri Tanzania. Wapo wachezaji wamejipatia umaarufu mkubwa hapa Tanzania licha ya kuwa huko walikotoka hawakufanya vizuri
Kama Yanga itamsajili Kambole basi atahukumiwa kwa kile ambacho ataifanyia Yanga sio kile alichofanya katika klabu nyingine