Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha siku ya Jumatano wanapata ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union na kuweza kutwaa ubingwa
Manara amesema Wananchi wameusubiri kwa hamu ubingwa huo wa 28 sasa ni kazi kwao kuhakikisha hawasubiri zaidi
Akihutubia katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Manara amesema licha ya dhamira yao ya kutwaa ubingwa, wataipa heshima klabu ya Coastal Union kwani wanatambua ni timu nzuri yenye hostoria kubwa na soka la Tanzania
Amesema wana uhakika wa kushinda ubingwa kwa asilimia 99 lakini bado hilo halijakamilika, wanataka likamilike Jumatano
"Tumebakiza michezo minne (4) ya ligi kuu ya Tanzania NBC, katika michezo 26 tuliyocheza tumekusanya alama 64, tukishinda michezo 20 na sare 6, kwenye mzunguko wa kwanza tulishinda michezo 12 na sare 3 pia kwenye mzunguko wa pili tumeshatoka sare michezo mitatu (3) na tunadaiwa ushindi wa michezo 4 ili tukusanye alama sawa na mzunguko wa kwanza"
"Nafasi yetu ya kushinda ubingwa ni kubwa sana kama 99%, bado hatujashinda ubingwa lakini nafasi ya sisi kuwa mabingwa ni kubwa sana, kwa mujibu ya msimamo wa ligi tunaitaji alama 3 ili tutawazwe kuwa mabingwa wa msimu huu"
"Huu ndiyo msimu wetu bora zaidi katika kipindi cha miaka 10 nyuma, baada ya kupoteza michezo miwili ya ligi ya mabingwa na ule mchezo wa Wiki ya Wananchi kutokea hapo utajapoteza mchezo wowote ndani ya dakika 90β mpaka hivi sasa"
"Jumatano ya tarehe 15/6/2022 ni siku yetu Wananchi, ni siku ambayo tunaenda kutengeneza historia endapo kama tutapata matokeo tutakwenda kushinda Ubingwa mara 28," alisema Manara