Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Nabi amesema Yanga itawakosa wachezaji watatu tu kutokana na sababu mbalimbali
Mlinda lango Djigui Diarra ataukosa mchezo huo kwa kuwa amefanya mazoezi siku moja na wachezaji wengine
Diarra alichelewa kurudi kutoka katika majukumu ya timu ya Taifa ya Mali
Nabi amebainisha kuwa nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ni majeruhi wakati Kibwana Shomari anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu
ADVERTISE HERE