Mayele, Fei Toto waibua shangwe Bungeni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jun 2022
Mayele, Fei Toto waibua shangwe Bungeni

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele na kiungo Feisal Salum wameibua shangwe kwa wabunge mara baada ya Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Mwigulu Nchemba kutaja majina yao.

Shangwe hilo limetokea jana Juni 14, 2022 bungeni wakati Mwigulu akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka 2022-2023.

Mara baada ya Mwigulu kutaja majina ya wachezaji hao wabunge walianza kushangilia kwa kupiga makofi.

"Nampongeza GSM kwa kurejesha furaha ya wananchi hasahasa kwa usajili wa Fiston Mayele. Mayele amekuwa maarufu kuliko Makatibu wenezi wa baadhi ya vyama vya Siasa" Waziri Mwigulu alisema

Dk Mwigulu pia aliweka utani kwa kumuomba radhi Waziri Mkuu kwa bao la Fei Toto alilowafunga Simba kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA jijini Mwanza

"Nachukua fursa hii kuwapongeza Yanga kwa mwenendo wao mzuri sana mwaka huu na nitumie fursa hii kumuomba radhi bosi wangu Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kitendo alichowafanyia  mwanangu Fei Toto kule Mwanza

"Mniwie radhi nilipompeleka Fei Toto Yanga sikujua atakuja kuwafanyia kitu mbaya hivi, mpaka nasikia anatafutwa maliasili eti kaua mnyama bila kibali"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’