Wakati Yanga ikiuanza msimu huu ilikuwa na nyota sita kutoka DR Congo na imemaliza msimu ikiwa na nyota sita kutoka DR Congo pia
Djuma Shabani, Yannick Bangala, Jesus Moloko, Heritier Makambo, Fiston Mayele na Chico Ushindi ambaye alitua mwezi Januari kuchukua nafasi ya Mcongomani mwenzake Mukoko Tonombe
Wapo waliobeza usajili huu wengine wakikejeli kuwa Yanga inasajili Wacongo kwa ajili ya kufungua bendi ya muziki na sio kucheza soka
Lakini baada ya wachezaji hawa kuwa na mchango mkubwa katika ubingwa wa Yanga msimu huu, kauli hizo zimepotea
Yanga ilifanya 'scouting' ya maana kuwanasa wachezaji hawa kwa ajili ya mpango wao wa kutwaa ubingwa msimu huu, WAMEFANIKIWA
ADVERTISE HERE