Tumeandaa sherehe kubwa ya Ubingwa - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2022
Tumeandaa sherehe kubwa ya Ubingwa - Manara

Msemaji wa Yanga Haji Manara ametoa shukrani kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi, wadhamini bila kuwasahau mashabiki kwa jitihada zao ambao zimewawezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Manara amesema haikuwa rahisi kutwaa ubingwa tena pasipo kupoteza mchezo, umoja na ushirikiano wao ilikuwa silaha kubwa kwao kufanikisha lengo waliloliweka

Manara amesema wapo waliowabeza wakati wakiitisha mikutano na wanahabari lakini matunda yake yameonekana kwani kwa mara nyingine Yanga imeongoza kuwa kuingiza mashabiki viwanjani

"Kwanza tunapenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, na pia tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi wetu, wadhamini pamoja na Mashabiki wetu wote. "

"Press nyingi ndiyo siri ya Yanga kufanikiwa msimu huu, ambapo Press hizo zimeleta mashabiki wengi Uwanjani na kuwapa morali wachezaji wapambane. Na niwaambie tumeongoza tena kuingiza mashabiki wengi uwanjani msimu huu bodi ya ligi itakuja kuthibitisha," alisema Manara

Manara amesema wamejiandaa kwa shamrashamra kubwa za ubingwa ambapo Juni 26 itakuwa siku maalum kwa mashabiki wa Yanga kote nchini wakiandaa mapokezi ya aina yake wakati kikosi kitakaporea na ubingwa kutoka mkoani Mbeya

Katika hatua nyingine Manara amethibitisha Yanga kujitoa kwenye shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na Azam Media

Manara amesema Yanga itatoa taarifa rasmi kuelezea sababu zilizopelekea wachukue uamuzi huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’