Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza kalenda ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kwa msimu ujao ambapo michuano hiyo itaanza August 12 2022
Taarifa iliyotolewa na CAF siku chache zilizopita, imebainisha kuwa michezo ya hatua ya awali mpaka makundi itapigwa kabla ya Novemba 18 ambapo michuano hiyo itasimama kupisha kombe la dunia
Hatua ya mtoano itaanza mwezi Februari 2023 baada ya michuano ya CHAN itakayofanyia Algeria
CAF tayari imewaagiza Wanachama wake kutuma majina ya klabu zitakazoshiriki michuano hiyo pamoja na usajili wa kila timu mwisho ni Juni 30
Ni wazi hakutakuwa na mapumziko kwani baada ya mchezo wa fainali kombe la FA (Julai 02) takribani wiki tano zitasalia kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ambao utapigwa August 12