Nabi atoa zawadi ya Ubingwa kwa familia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2022
Nabi atoa zawadi ya Ubingwa kwa familia

Kocha mkuu wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga, Mohamed Nasreddine Nabi amesema ubingwa huo ni zawadi kwa familia yake ambayo imekuwa ikimfariji mara kwa mara licha ya kuwa mbali nayo

Yanga juzi iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union na kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kufikisha pointi 67 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote, ikiwa imecheza mechi 27 zikibaki tatu.

Mabao ya Yanga yakifungwa na Fiston Mayele aliyetikisa nyavu mara mbili na Ushindi Chiko, mchezo ukipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Nabi alisema ilikuwa safari ndefu hadi kufanikiwa kutwaa Kombe hilo.

"Nimefurahi kupata ubingwa, haikuwa kazi rahisi nawapongeza wachezaji wangu pamoja na Uongozi wa Yanga kwa ushirikiano walionionesha hadi leo (juzi) tumefanikiwa kupata ubingwa," alisema Nabi.

Alisema mechi zote ambazo wamecheza zilikuwa ni kama fainali na kudai kila timu ambayo walicheza nayo ilikuwa inawakamia kwa kiasi kikubwa, lakini walikuwa hawawapi nafasi.

Alisema watauendeleza ushindani huo huo kwenye michezo mitatu iliyobakia ili wamalize msimu huu wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Amvulia kofia Sureboy

Nabi alimsifia kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' kuwa ni usajili ambao ameupenda kwa sababu ni mchezaji alioyeongeza nguvu ndani ya kikosi cha timu hiyo licha ya nyota huyo kuhitaji kuongezewa vitu kidogo ili kuwa bora zaidi.

"Sure Boy ni moja ya usajili mzuri ambao Yanga walifanya, ameleta nguvu ndani ya kikosi na amesaidia sana safu ya kiungo"

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’