Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema baada ya msimu kumalizika, wataelekea nje ya nchi kuweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu ujao wa mashindano
Ligi Kuu ya NBC itamalizika Juni 29 lakini Yanga itamaliza msimu kwa mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa Julai 02 uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Hersi ambaye ni mgombea pekee wa Urais wa Yanga, amesema wanatambua michuano ya ligi ya mabingwa inatarajiwa kuanza mwezi August hivyo watatoa muda mfupi wa mapumziko kwa wachezaji kabla ya kuelekea nje ya nchi kuweka kambi
"Ligi Kuu itamalizika Juni 29 lakini sisi tuna mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Coastal Union Julai 02, baada ya mchezo huo tutatoa mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji wetu"
"Hatutakuwa na muda mrefu sababu ligi ya mabingwa mechi za awali zitaanza kati ya August 12-14 hivyo mpaka kufikia Julai 15 tunapaswa kuanza maandalizi. Tutakuwa na takribani wiki tatu za kambi ambayo tutaweka nje ya nchi," alisema Hersi
Hersi amedokeza kuwa kilele cha wiki ya Mwananchi huenda ikawa August 06