Mshambuliaji mpya wa Yanga Lazarus Kambole amesema atapendelea kutumia jezi namba saba katika kikosi cha Yanga
Kambole aliyesajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Kaizer Chiefs akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika, alikuwa akivaa jezi namba saba wakati yuko Kaizer na hata anapokuwa timu ya Taifa
Jezi namba saba inatumiwa na kiungo Mapinduzi Balama ambaye ni wazi Yanga huenda ikamtoa kwa mkopo ili apate kuimarika zaidi baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa miezi 18
Wananchi wanakumbuka msimu uliopita jezi namba saba ilitumiwa na Fiston Abdulrazak ambaye hata hivyo hakuweza kuwapa furaha waliyotarajia
Wakati anaitumikia Zesco United, Kambole alikuwa akivaa jezi namba tano
Namba ya jezi haichezi mpira lakini wachezaji wengi huamini akivaa jezi namba flani inamuongezea bahati
Lakini kwa wengine namba za jezi wanazovaa zinabeba kumbukumbu muhimu katika maisha yao