Uongozi wa Yanga umethibitisha kupokea barua kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) juu ya kusogezwa mbele kwa mwezi mmoja kuanza kwa michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika
Michuano hiyo sasa itaanza Septemba 09 badala ya August 12 iliyokuwa imetangazwa awali na Shirikisho hilo
Mabadiliko hayo pia yamepelekea kusogezwa mbele kwa dirisha la usajili wa CAF ambalo sasa litafunguliwa August 01 mpaka August 15 kwa timu kusajili pasipo faini
Baada ya August 15, timu zitaruhusiwa kuandikisha wachezaji kwenye mfumo ndani ya siku 10 kwa kulipa faini ya dola 5,000 kwa kila mchezaji
Hii ni habari njema kwa Wananchi kwani sasa hata yule 'mtukutu' waliyetaka kumbania ataweza kusajiliwa katika kikosi cha ligi ya mabingwa!
ADVERTISE HERE