Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga jioni ya leo majira ya saa 12 wanashuka kunako uwanja wa Benjamin Mkapa kuumana na Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Ni mchezo wa kukamilisha ratiba kwa Yanga kwani Wananchi tayari wameweka 'kibindoni' ubingwa wa 28
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na dhamira moja tu, kupata ushindi ili kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo msimu huu
Katika mchezo huo huenda kocha Nasreddine Nabi akatoa fursa kwa baadhi ya nyota ambao wamekosa nafasi ya mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza
Aidha, itakuwa nafasi kwa mshambuliaji Fistorn Mayele kujiimarisha kwenye mbio za kuwania ufungaji bora msimu huu
Mayele anachuana vikali na George Mpole wa Geita Gold wote wakiwa wamepachika mabao 16
Mchezo utapigwa kuanzia saa 12:30 jioni