Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wamepokea ofa kutoka klabu mbalimbali kuwataka wachezaji wao lakini hawatakuwa tayari kuwauza wachezaji hao chini ya thamani zao
Manara ametoa mfano wa kiungo mshambuliaji Feisal Salum 'Fei Toto' kuwa thamani yake sio chini ya Tsh Bilioni moja hivyo Yanga haitamuuza chini ya bei hiyo
"Tunao wachezaji wazawa ambao wana thamani kubwa, mfano Feisal thamani yake sio chini ya Bilioni 1. Zipo ofa nyingi tumepokea lakini tumekubaliana huyu Feisal tutafikiria kumuuza kama kuna timu italeta sio chini ya fedha za Kitanzania Bilioni moja," alisema Manara
Klabu ya Smouha ya Misri inatajwa kuwasilisha ofa kutaka kumnunua Feisal lakini ni wazi ofa yao haijawashawishi Yanga
Feisal ni miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha Nasreddine Nabi kuelekea michuano ya Kimataifa msimu ujao