Jumapili Juni 26 itakuwa siku maalum kwa Wananchi kote nchini kwani shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu msimu huu zitafanyika
Zimeandaliwa sherehe kubwa za ubingwa jijini Dar es salaam ambapo msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wameagiza basi maalum kwa ajili ya kuwabeba wachezaji, basi hilo litazunguuka jiji lote la Dar es salaam
Manara amesema baada ya mapokezi ya kikosi kikitokea mkoani Mbeya ambako watakabidhiwa ubingwa wa ligi kuu baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City, msafara utaanzia uwanja wa Ndege ukiongozwa na basi hilo pamoja na farasi
"Mapokezi ya kombe yatafanyika pale JNIA, kutakuwa na basi maalum kutoka nje ya nchi, kutakuwa na magari mengi maalum lakini pia tumeandaa farasi watakuwepo pale"
"Tutapita route nyingi ikiwa ni pamoja na Msimbazi lakini mwisho tutaishia kaunda Jangwani, pale sasa kutakuwa na pilau watu watakula na kusaza," alisema Manara