Baada ya safari ndefu lakini yenye mafanikio, hatimaye Yanga iko tayari kupokea ubingwa walioupigania kwa dhati msimu huu
Siku ya kesho Jumamosi, Juni 25 2022, itaingia kwenye historia kuwa Yanga ilikabidhiwa ubingwa wa ligi kuu waliotwaa msimu huu ambao ni ubingwa wa 28 kwao
Ni rekodi kwa Yanga kwani ni miaka 56 tangu Ligi Kuu ilipoanzishwa Tanzania Bara na Yanga imeshinda ubingwa nusu ya muda wote na nusu nyingine zikigawana timu nyingine
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema haukuwa msimu mwepesi lakini Yanga imestahili kuvaa medali kwani wameonyesha kwa vitendo kuwa walistahili kuwa mabingwa
ADVERTISE HERE