Aliyekuwa kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane amepongeza tukio la shamrashamra za ubingwa lililofanywa na klabu ya Yanga akilitaja tukio hilo kuwa linapaswa kuwa mfano kwa klabu nyingine barani Afrika
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter, Mosimane amebainisha kuwa Yanga wamedhihirisha kuwa hata Waafrika wanaweza kufanya 'parade' ya ubingwa kama inavyofanyika barani Ulaya
"Tunahitaji kuona matukio kama haya zaidi barani Afrika kwani yanaonyesha kwa kiasi gani mashabiki wa soka wanazipenda timu zao," aliandika Mosimane
ADVERTISE HERE