Baada ya shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu zilizosimamisha jiji la Dar es salaam na kuitikisa Afrika, kikosi cha Yanga kimerejea kambini kukamilisha maandalizi ya mchezo wa mwisho katika ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar
Kesho Jumatano, Juni 29, Ligi Kuu ya NBC itahitimishwa Yanga ikishuka dimba la Mkapa kuwakaribisha Mtibwa Sugar ambao bado hawana uhakika na usalama wao wa kubaki ligi kuu
Afisa Habari wa Yanga Yanga Hassani Bumbuli amesema bado wana kiu ya kusaka rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa kimashindano msimu huu
"Ni mchezo muhimu sana wa kuandika historia,kuna timu ziliweka historia nyuma lakini sisi hatujapoteza katika mashindano yoyote na tunataka kuweka historia ya kumfunga Mtibwa Sugar ili twende tukamalize msimu vizuri Arusha kwenye fainali ya FA, "amesema Bumbuli