Bodi ya Ligi imetangaza kuwa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/23 itaanza August 17 2022 na ikitarajiwa kumalizika May 2023
Mtendaji Mkuu wa Ligi Almas Kasongo amesema mchezo wa Ngao ya Jamii unaoashiria ufunguzi wa ligi hiyo utapigwa August 13
Mchezo huo utazikutanisha bingwa wa ligi kuu msimu huu (Yanga) na bingwa wa michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Kama Coastal Union itatwaa kombe la FA, basi itakutana tena na Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii lakini kama Yanga watatwaa taji la FA, basi kwenye Ngao ya Jamii watakutana na watani zao Simba ambao wamemaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi
ADVERTISE HERE