Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kitawakosa takribani wachezaji nane kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utahitimisha msimu wa ligi kuu siku ya kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Nabi amesema maandalizi ya kikosi chake yamekamilika lakini kutokana na sababu mbalimbali kama kutumikia adhabu na wengine kuwa majeruhi, wachezaji hao watakosekana
Nabi amesema pia wataingia katika mchezo huku wakifahamu wanasiku tatu tu kuelekea mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa Julai 02 uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Nabi amesema wanatarajia mchezo wenye ushindani mkali kwani wanafahamu Mtibwa Sugar wanahitaji ushindi ili kujihakikishia kubaki ligi kuu na wao hawatapenda kupoteza mchezo wa mwisho baada ya kucheza bila kupoteza msimu mzima