Wakati ligi kuu ya NBC ikihitimishwa leo, mbio za kuwania ufungaji bora zimebaki kwa washambuliaji wawili Fiston Mayele wa Yanga na George Mpole wa Geita Gold
Mayele na Mpole wote wamfunga mabao 16 kuelekea michezo ya kuhitimisha msimu jioni ya leo
Mayele atakuwa na kikosi cha Yanga jijini Dar es salaam wakiikabili Mtibwa Sugar kunako dimba la Benjamin Mkapa wakati Mpole atakuwa na Geita Gold kule mkoani Tanga wakiikabili Coastal Union

Mpaka sasa Mayele yupo juu ya Mpole kwa kuwa na assist nyingi (5) wakati Mpole ana assist nne
Katika msimu huu Mayele hajafunga bao la mkwaju wa penati wakati Mpole amefunga mabao matatu ya mikwaju ya penati
Kama wachezaji hao watafungana idadi ya mabao baada ya michezo ya leo, basi watagawana zawadi ya ufungaji bora
Kwa hakika ulikuwa msimu mzuri sana kwa Mayele na kikosi cha Yanga wakifanikiwa kutwaa ubingwa, pia ulikuwa msimu mzuri kwa Mpole na Geita Gold wakiwa na uhakika wa kumaliza katika nafasi nne za juu
Geita Gold wana nafasi kubwa ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, hasa kama Yanga watatwaa taji la FA