Winga mtukutu raia wa Ghana Bernard Morrison yuko nchini kuagana na timu yake ya zamani Simba aliyoitumikia kwa misimu miwili
Pamoja na kutaja sababu iliyomfanya aachane na Simba, Morrison amesema mkataba wake na Simba ulimalizika baada ya mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza hapo juzi
"Mkataba wangu na Simba unapaswa kumalizika mwishoni mwa msimu hivyo baada ya mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza mimi ni mchezaji huru," alisema Morrison
Morrison ametaja sababu ya kuachana na Simba ni suala la maslahi huku akibainisha kuwa uongozi wa timu hiyo ulimsimamisha na kumpa matatizo ya kifamilia (ambayo hakuwa nayo) baada ya kugoma kusaini mkataba mpya
Morrison amesema amerudi Tanzania na ataendelea kucheza hapa ikielezwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga