Wakati Haji Manara alipojiunga Yanga na kuja na 'slogan' ya The Return of Champions wapo waliobeza lakini leo msemo huo umedhihiri
Yanga imetwaa taji la tatu msimu huu, ikiweka rekodi ya kutopoteza mchezo katika michuano yote ya ndani
Ndio! Mabingwa wamerejea na moto huu hakuna wa kuuzima, Wananchi wanaweka kabatini mataji matatu msimu huu
Ubingwa huu wa FA una maana sasa Geita Gold wataungana na Azam Fc kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika wakati Yanga wakiwa mabingwa wanakwenda kucheza michuano ya ligi ya mabingwa wakiwa na watani zao Simba ambao msimu huu wametoka 'patupu'
Mchezo wa Ngao ya Jamii kukaribisha msimu ujao ni kati ya Yanga dhidi ya Simba na utapigwa August 13
ADVERTISE HERE