Msimu umemalizika kwa Yanga kushinda mataji yote yaani Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hapo jana
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said amesema wamekamilisha malengo waliyojiwekea kwa asilimia 100, wanajipanga kuhakikisha msimu ujao wanaendeleza mafanikio haya yaliyopatikana msimu huu
Wachezaji sasa wanakwenda mapumziko ambapo watarejea kambini kabla ya Julai 15 kuanza maandalizi ya msimu ujao
Msimu wa 2022/23 utaanza August 13 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba
Habari njema, michuano ya ligi ya mabingwa itaanza mwezi Septemba wakati ligi kuu ya NBC ikiwa tayari imechanganya. Ligi Kuu itaanza August 17
Yanga itaingia katika michuano hiyo ikiwa imeiva sawasawa
ADVERTISE HERE