Morrison ahukumiwe kwa kazi yake uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2022
Morrison ahukumiwe kwa kazi yake uwanjani

Usajili wa winga Bernard Morrison unatajwa kuwa mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi kwa asilimia 100

Morrison ni mchezaji anayezungumzwa zaidi kutokana na kipaji chake pengine jambo pekee linalowapa wananchi mashaka ni nidhamu yake

Hata hivyo Morrison anarejea katika kikosi cha Yanga ambacho ni tofauti kabisa na kile ambacho yeye alikuwa sehemu yake kwa miezi sita

Morrison ametua Yanga ambayo msimu huu imeshinda mataji yote tena pasipo kupoteza mchezo

Yanga ambayo imejipambanua, haitegemei mchezaji mmoja. Yanga ambayo Kocha Nabi ndiye msimamizi mkuu wa masuala ya nidhamu ya wachezaji, na hana masihara

Ni wazi yapo masharti ambayo Yanga wameyaweka kwenye mkataba wa Morrison ili kuhakikisha wanamdhibiti

Lakini pia hata kwa Morrison mwenyewe atapaswa kupambana ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza

Hakuna haja ya kufanya utabiri, msimu utakapoanza, Morrison atahukumiwa kwa kile anachofanya uwanjani na sio historia na matukio yake ya nyuma

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’