Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Malangwe Mchungahela ametangaza Uchaguzi Mkuu wa Yanga ambao ulipangwa kufanyika Julai 10, sasa utafanyika Julai 09
Mchungahela amesema mabadiliko hayo yametokana na taarifa ya Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) kutangaza kuwa Julai 10 ni sikukuu ya Eid Al Haji
Kampeni za uchaguzi zimefunguliwa rasmi leo na zitafika tamati Julai 08
Mchungahela pia ametangaza kurejeshwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi Mustapha Himba anayewania Ujumbe Kamati ya Utendaji baada ya kushinda rufaa yake
Matawi ambayo hayakuwa yamekamilisha michakato ya uchaguzi yanapaswa kuwasilisha orodha ya wajumbe watano ambao watashiriki uchaguzi
Matawi ambayo hayatawasilisha majina mapema, wajumbe wake hawataruhusiwa kupiga kura
ADVERTISE HERE