Dk Msolla asisitiza umoja, ushirikiano Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2022
Dk Msolla asisitiza umoja, ushirikiano Yanga

Mwenyekiti wa Yanga anayemaliza muda wake Dk Mshindo Msolla amesisitiza mshikamo miongoni mwa Wanayanga ili kuhakikisha wanayalinda mafanikio waliyopata na kuongeza mafanikio zaidi

Dk Msolla amesema baada ya mabadiliko ya Katiba ambayo yamewezesha mfumo mpya, hakuona sababu ya kuwania nafasi ya Urais kwani yeye ni muumini wa utawala bora

Aidha Dk Msolla amesema amejiridhisha na uwezo wa wagombea waliojitokeza, wanaweza kuifikisha Yanga kule ambako kila mmoja anatamani

Dk Msolla amesema hajaondoka Yanga kwa ubaya, bali ametimiza ahadi aliyotoa wakati akiwania Uwenyekiti wa klabu ya Yanga

"Sikuona sababu ya kurudisha fomu baadhi ya kujiridhisha kuwa wagombea waliojitokeza wanatosha"

"Kwa wale mnaokumbuka wakati wa kampeni nikiwa nawania Uwenyekiti, nilisema kama nitafanikiwa suala la Mabadiliko, ndani ya mwaka mmoja au miwili nitaachia madaraka kwa kuwa najua nitakuwa nimeipeleka klabu yangu katika sehemu sahihi," alisema Dk Msolla

Dk Msolla amewaasa wagombea kutochafuana wakati wa kampeni, wahakikishe wanavunja makundi baada ya uchaguzi

"Nawaasa wagombea, hakuna sababu ya kuchafuana wakati wa kampeni, Nalisema hili kutokana na uzoefu wangu, wakati nikiwa nagombea nilichafuliwa sana, hakuna sababu ya kufanya hivyo"

"Baada ya uchaguzi tuhakikishe tunaendelea kuwa wamoja kwa kuvunja makundi yetu. Ni umoja wetu ndio utakaofanya klabu yetu iweze kusonga mbele"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
20m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’