Afe kipa, afe beki tutajenga uwanja - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2022
Afe kipa, afe beki tutajenga uwanja - Injinia Hersi

Mgombea Urais klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema katika kipindi chake cha uongozi kama atachaguliwa kuiongoza Yanga, atakamilisha ujenzi wa uwanja wa Kaunda ambao utachukua mashabiki 20,000

Hersi amesema hitaji namba moja kwa Yanga sasa ni kuwa na uwanja wao wa mechi kwani hawana changamoto na uwanja wa mazoezi

"Nimeahidi, afe beki afe kipa, katika muda wangu wa uongozi tutajenga uwanja ambao utachukua mashabiki 20,000. Wapo wanaohoji kwa nini tusijenge Kigamboni ambako tuna eneo kubwa, niwaambie tuna eneo zuri pale Jangwani ambalo ni rahisi kufikika kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam"

"Tumejipanga kulikamilisha hili na niwaambie tu baada ya uchaguzi kupita, tutawaleta wataalam wafanye 'feasibility study' ili kazi ianze mara moja," alisema Hersi 

Katika hatua nyingine, Injinia Hersi amesema wamefanya usajili wa nyota watano wa kigeni ambao wataongeza ushindani katika kikosi

Hersi amesema watatambulisha usajili wa wachezaji wengine watatu waliobaki huku akiwahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa wameleta watu kwelikweli

"Tunaleta kiungo mshambuliaji ambaye kacheza La Liga katika klabu ya Rayo Vallecano, tunashusha moja ya walinzi bora wa kushoto katika bara hili la Afrika, na huyo mwingine atakuwa funga kazi, CV yake ni kubwa sana (kacheza ligi kuu Uingereza!), " alitamba Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
44m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’