Mshambuliaji Obrey Chirwa kwa mara nyingine amedhihirisha umuhimu wake kwenye kikosi cha Yanga baada ya leo kuingoza kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji.
Chirwa amefunga mabao matatu 'hat-trik'.
Hiyo ni hat-trik yake ya pili msimu huu. Kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ambao Yanga ilishinda kwa mabao 5-0, Chirwa alipiga hat-trik pia.
Sasa amefikisha mabao 10, yuko nafasi ya pili katika orodha ya vinara wa upachikaji mabao nyuma ya Emanuel Okwi mwenye mabao 12.
Chirwa ana mchango mkubwa katika kikosi cha Yanga kwa sasa hilo halina ubishi.
Akishirikiana vizuri na Buswita, kwa pamoja na wachezaji wengine kikosini, wanaifanya Yanga kuwa moto wa kuotea mbali.
Bila shaka mchakato wa kumuongezea mkataba utafanyika mapema ili kuepuka kumpoteza mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utamalizika.
Umri wake wa miaka 23 bado unamruhusu kuendelea kuwepo Jangwani kwa miaka mingi!

ADVERTISE HERE