Katika msimu uliopita, Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao GSM wametoa misaada mbalimbali katika kila mkoa ambao walikwenda kucheza
Hata baada ya msimu kumalizika, baadhi ya wachezaji wa Yanga wametumia mapumziko yao kusaidia jamii zao
Tumemshuhudia Deus Kaseke, akitoa misaaa Mbeya, Dickson Job na Kibwana Shomari wakaandaa mechi ya hisani mkoani Morogoro na baadae kutoa misaada kwa wenye uhitaji
David Bryson nae ametumia mapumziko yake kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalum katika jamii anayotoka
Hii ni ndio maana halisi ya kuwa mchezaji wa Yanga, timu ya Wananchi




ADVERTISE HERE