Baada ya kumnasa aliyekuwa mlinzi wa kulia wa Yanga Paulo Godfrey 'Boxer', Singida Big Stars wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Yassin Mustafa, ambaye nae amemaliza mkataba na klabu ya Yanga
Yassin ni miongoni mwa wachezaji ambao hawatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya mkataba wake kufika tamati
Yassin ameitumikia Yanga kwa misimu miwili, msimu wake wa mwisho haukuwa na mafanikio sana kutokana na kuandamwa na majeraha
Hata hivyo ameshiriki kikamilifu katika kikosi cha Yanga kilichotwaa mataji matatu msimu uliomalizika
Wananchi wataendelea kuukumbuka mchango wake
ADVERTISE HERE