Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza klabu ya soka ya Wydad Athletic ya Morocco kumlipa Mchezaji Mtanzania Simon Msuva zaidi ya dola za kimarekani laki saba (Tsh. zaidi ya bilioni 1.6)
Ni baada ya Msuva kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Wydad. Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake December 2021 kutokana na kuidai Wydad malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili
Kulingana na AyoTV, FIFA imeiamuru Wydad wamlipe Msuva kiasi hicho cha pesa pamoja na fidia
ADVERTISE HERE