Usiku wa kuamkia leo Yanga ilitambulisha mchezaji wanne kusajiliwa na mabingwa hao wa Tanzania, Mcongomani Joyce Lomalisa Mutambala
Mutambala ametua kwa Wananchi kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji wa nne kusajili katika dirisha hili la usajili baada ya Lazarus Kambole, Bernard Morrison na Gael Bigirimana
Bado mchezaji mmoja tu ambaye Yanga wakimtambulisha watafunga usajili wao kwa wachezaji wa kigeni
Huyo si mwingine, ni Stephane Aziz Ki, nyota aliyeanzia soka lake katika Academy ya Rayo Vallecano kule Hispania
Aziz Ki ni mchezaji ambaye amezungumzwa zaidi katika dirisha hili la usajili, bila shaka utambulisho wake utakuwa wa kipekee
Zilipoanza tetesi za Yanga kumuwania nyota huyu, wapo wachambuzi wa soka hapa Tanzania na hata wengine kutoka nje ya nchi walibeza
Hata zilipovuja picha Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akiwa na Aziz Ki pamoja na mama yake wapo waliodai kuwa picha hizo zilitengenezwa (feki) na wengine kudai Hersi alisafiri Ivory Coast kwenda kupiga picha tu na mchezaji huyo ili arahisishe ushindi wake katika uchaguzi
Bila shaka utambulisho wamchezaji huyu atawafunga midomo wale waliokuwa wakimbeza Injinia Hersi ambaye Wanachama wa Yanga wamemchagua kuwa Rais wao sio kwa sababu amemsajili Aziz Ki
Lakini pia utakuwa ujumbe kwa wale wanaoibeza Yanga, wajue kuwa mambo yamebadilika, Yanga ya sasa imedhamiria na tayari kurejesha heshima yake kwenye soka la Kimataifa baada ya kufanya hivyo hapa nyumbani kwa kushinda mataji yote katika msimu uliomalizika